KUFUATIA mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Msimu wa Pili wa Coke Studio Africa, Kampuni ya Coca-Cola kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Kenya, inayo furaha kutangaza kuanza tena msimu wa tatu wa burudani ya muziki maarufu kwa jila la Coke Studio Africa. msimu huu utajumuisha wanamuziki wakali 26 barani Afrika huku nyimbo mpya 52 kutumbuizwa ikiambatana na maonyesho 9 ya wanamuziki wanaotamba hapa duniani.
Maonyesho hayo ya muziki ya Coke Studio Africa ni tofauti na mengine ya aina hiyo yanayolenga zaidi kupatikana mshindi. Badala yake, maonyesho haya yanalenga kujumuisha pamoja vipaji tofauti vya wanamuziki mbalimbali kutoka barani Afrika. Aidha, yanatoa fursa kwa wasanii wanaochipukia kufanya pamoja kazi zao na wanamuziki nguli wa ndani na wale wa ngazi za kimataifa
Ali Kiba
Msimu huu
unaozinduliwa utawakutanisha wanamuziki kutoka katika nchi za Tanzania,
Msumbiji, Kenya, Uganda na Nigeria, na kwa mara ya kwanza wasanii hawa
wataweza kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki kwa kushirikiana katika
staili ya kipekee ijulikanayo kama mash-ups – ambayo inatawala kwa sasa
katika tasnia ya muziki duniani. “Kufurahia muziki wa Kiafrika” ikiwa
ndiyo kiini kikuu cha burudani hiyo, msimu huu mpya wa Coke Studio
Africa utawakutanisha wasanii maarufu ambao wameonyesha mafanikio
makubwa katika kazi zao, na pia maonyesho hayo yatawaleta pamoja wasanii
nyota wanaochipukia katika ulimwengu wa muziki.
Chini ya
ushirikiano huo mpya na Kampuni ya Coca-Cola, Shirika la Ndege la Kenya
kwa upande wake litawasafirisha wasanii wote na waandaaji wa muziki
wanaoshiriki katika Msimu wa Tatu wa Coke Studio Africa. Mpango huo wa
ushirikiano wa makampuni haya makubwa unatokana na imani ya kwamba hatua
hiyo itajenga msingi wa ubia muhimu wa kufanya kazi kwa pamoja.
Vanessa Mdee
Akizungumzia juu
ya Coke Studio Africa Msimu wa Tatu, Meneja Bidhaa wa Coca-Cola
Tanzania, Maurice Njowoka alisema: “Lengo letu ni kuufanya na kuwezesha
namna ambayo muziki unavyoweza kuchukua nafasi katika kukonga nyoyo za
watu katika Bara letu. Coke Studio Msimu wa Tatu si kwa ajili ya
kuwakutanisha tu wanamuziki wa Afrika, bali pia maonyesho haya yanatoa
fursa ya pekee ya ushirikiano ambao ni imani yetu kuwa wateja wetu
pamoja na umma kwa ujumla wangependa kuusikia.”
Bwana Njowoka
alisema kwamba, msimu huu wa Coke Studio Africa Msimu wa Tatu
unatarajiwa kuwa na mambo makubwa na mazuri zaidi na utatoa fursa ya
kipekee kwa kila mtu kuburudika zaidi. Miongoni mwa nyota watakaotoa
burudani msimu huu ni pamoja na Ali Kiba, Vanessa Mdee Ben Pol na Fid Q
kutoka Tanzania.
Wengine ni
AVRIL, Wangen, The Unstoppable Elani na Juacali kutoka Kenya il-hali kwa
mara ya kwanza Malkia wa Afrika, 2Face Idibia, ataonyesha vitu vyake
motomoto akiungana na nyota wengine kama vile Yemi Alade. Magwiji
wengine katika tasnia hiyo ya muziki watakaokuwapo ni pamoja na Dr. Jose
Chameleone, Neyma, Dama Do Bling kutoka Msumbiji.
Mkuu wa Idara ya
Masoko wa Shirika la Ndege la Kenya, Jacquie Muhati, alisema ya kuwa
ushirikiano kati ya shirika lake na Kampuni ya Coca-Cola utatoa fursa
kwa wasanii hao wa Afrika kufurahia huduma nzuri za usafiri zinazotolewa
na shirika hilo. “Hii ni fusa kubwa kwetu kulitangaza bara letu kupitia
huduma zetu bora zinazotolewa katika ndege zetu. Tumedhamiria kukuza
vipaji vya wasanii wachanga barani Afrika.”
Bi. Muhati
aliongeza kwa kusema kuwa ushirikiano huo ni uthibitisho wazi
unaodhihirisha jinsi shirika hilo linavyojitolea katika kukuza fani ya
muziki barani Afrika, na pia utashi na mapenzi makubwa ya shirika hilo
kuona kuwa linakuwa sehemu ya kukuza vipaji na maendeleo ya wasanii wa
Afrika.
Mwanamuziki
ambaye ni mshindi wa tuzo ijulikanayo kama Grammy Award ambaye pia ni
mwandaaji wa muziki, Zwai Bala, magwiji wa Kwaito kutoka Afrika Kusini,
Kikundi cha TKZee, wataongoza maonyesho hayo ya muziki. Brett Lotriet,
ambaye ni mwandaaji na mwongozaji wa kimataifa wa maonyesho ya TV ni
miongoni mwa vinara ambaye ataoongoza uandaaji wa maonyesho ya Coke
Studio Msimu wa Tatu kadri matukio yatakavyokuwa yakitokea.
Wanamuziki wakiwa
pamoja na bendi za wasanii nyota wa ndani watatoa nyimbo mpya kila wiki
ambazo zitaandaliwa na waandaaji wa ndani na wale wa kimataifa. Baadhi
ya waandaaji ni pamoja na Jaaz Odongo, Eric Musyoka na Kevin Provoke
kutoka Kenya, Cobhams Asuquo, Masterkraft na Chopstix kutoka Nigeria,
Owour Arunga kutoka Marekani, Nahreel kutoka Tanzania na Silvastone
kutoka Uingereza. Yakiwa yamesheheni nyota wakali wa muziki, maonyesho
haya ya msimu huu yataufanya muziki wa Afrika ukue na kufikia katika
hatua mpya ya juu zaidi.
Kwa Mhariri:
Mash-up ni wimbo
au tungo ya muziki ambao umeandaliwa kwa kuchanganya nyimbo mbili au
zaidi zilizorekodiwa mapema, na kwa kawaida hufanywa kwa kuchanganya
nyimbo hizo ili kutoa kitu kipya kinachowajumuisha wanamuziki wote
wahusika katika nyimbo zilizochanywa.
Credit: Mtata kwa mtaa
0 comments :
Post a Comment