News
Loading...

HAYA NDIYO ALIYOSEMA FID Q JUU YA KUSHINDANISHWA NA JOH MAKINI

 
Fid Q na Joh Makini ni rappers ambao wamekuwa wakichukuliwa kama hawaivi 
chungu kimoja, na wakati mwingine wamekuwa wakishindanishwa na mashabiki wanaotaka 
kujua nani mkali zaidi ya mwenzake.
 
Fareed “Fid Q” Kubanda ametoa mtazamo wake wa kile anachodhani kuwa sababu ya 
mashabiki wa muziki wa Hip Hop kumshindanisha na rapper mwenzake Joh Makini kwenye 
mitandao.
“Labda ni kwasababu (Joh) anaweza akawa ni msanii ambaye
 anafanya vizuri kwahiyo wanakuwa wanamshindanisha na msanii mwenzake mwingine (Fid)  
ambaye anafanya vizuri, lakini sidhani kama kuna kitu personal na siko katika position 
kuamini mi nahitaji kushindanishwa na Joh.” Alisema Fid kupitia 255 ya XXL ya Clouds 
Fm. 
 
Fid amesema kuwa yeye ni msanii ambaye hawezi kushindanishwa na msanii mwingine 
yeyote kutokana na kile anachokifanya kuwa tofauti na wanachofanya wasanii wengine wote,
na pale anaposhindanishwa huwa anaona kama amedharaulika.
“Nadhani wanaoshindanisha wajifunze kuwa wanafatilia watu wanaotaka 
kuwashindanisha kwanza, mi nadhani niko tofauti kidogo na wanamuziki wengi sana ambao 
wanafanya Hip Hop na hiyo haijalishi kama ngoma zangu zinapigwa sana redioni au 
hazipigwi. Kibongobongo kiukweli mi sidhani naweza kushindanishwa na mtu na wala siwezi 
kujisikia vizuri, na mara nyingi naposhindanishwa na mtu naona kama nimedharaulika hivi,
sio kwasabbu huyo mtu mwingine ni dhaifu No!, kwasababu mi nafanya kitu cha tofauti
sana…nazingatia zaidi uandishi, nafanya show mpaka kesho na ngoma kama dotcom, 
dotcom ni ngoma ambayo nimeitoa 2003, 2004. Katika show zangu hizo hizo napigaga 
Mwanza Mwanza ambayo imetoka 2005 ilikuwa nyimbo bora ya Hip Hop…saizi ni 2015
 unaongelea miaka tisa iliyopita na zaidi, basi hebu tuangalie basi na hao wengine ambao 
wanataka kunishindanisha nao wana vibao vyao vina miaka hiyo tisa ambavyo wanaweza 
kufanya sasa hivi vingapi?”
Kuhusu kama amewahi kuwa na matatizo yoyote na Joh Makini:
“Sijawahi kuwa na matatizo na Joh Makini, nadhani matatizo yanayosikika kwa 
watu.
 
Unajua fans wana vitu vyao, ukiingia sehemu mara utakutana na mtu kaweka picha sijui
Fid Q vs Joh Makini nani noma, nadhani vitu kama hivyo ndo waga vinatengeneza chokochoko nyingi
 nyingi ambavyo mtu kama sio mtu wa kufikiria vyema unaweza kuchukulia personal.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment