Hii ni sehemu kidogo ya status ya Adebayor kuhusu kaka yake Kola
Leo nimeamua kuleta part 3 ya story yangu. Hii ni kwasababu kaka
yangu Kola Adebayor na ndugu zangu wameamua kuzungumzia mambo ya familia
kwenye social media, kutuma baria kwenda kwenye club na radio.
Ningeweza kuandika kitabu na kuuza lakini nimeamua ku-share na wewe
hapa.
Miaka 25 iliyopita kaka yangu mkubwa Kola alienda ujerumani na kuwa
tumaini kubwa kwa familia yetu. Wote tuliamini angeweza kubadilisha
maisha ya familia yetu. Miaka baada ya yeye kuondoka Togo bado hatukua
na umeme wala simu, Kama angetaka kuongea na sisi alikua anapiga simu
kwenye hotel inaitwa Atlantic Hotel ambayo ilikua karibu na nyumbani
kwetu.
Nilivyopata nafasi ya kwenda kucheza mpira France kwa mara ya kwanza,
tuliitaji pesa kwa ajili ya ticket ya ndege na gharama nyingine. Kaka
yangu hakupatikana kusaidia katika hili, mungu pekee anajua alichokua
anakifanya huko Ujerumani.
Nilivyofika Ujerumani nilijaza makaratasi yote na timu ikaniruhusu
kukaa kwenye academy. Baada ya miezi michache Kola akataka kunitembelea,
nilikua nakaribia kuishiwa na pesa na nilikua naishi kwenye academy.
Kwa hiyo nikaamua kuazima pesa ili kulipia hotel yake. Wakati huo
mchezaji mwenzangu Sega N’diaye kutoka Cameroon alikua na pesa za
kutosha akaniazima pesa. Pia ikabidi niazime pesa zaidi ili niweze kumpa
Kola atumie kwenye safari yake ya kurudi Ujerumani.
Baada ya miaka michache mambo yakaanza kwenda vizuri, nashukuru mungu
nikasaini mkataba na Mets.Tangu siku hiyo kaka yangu alikua
anawasiliana na mimi muda wote ukifika muda wa kulipia bili zake za
mwezi.Kuna muda alikua anasema kwamba mwanae anaumwa, so ikabidi nizoee
tu
Nikawa na bahati zaidi ya kupata ofa kutoka Monaco na nikasaini
mkataba nao. SIku moja Kola na marehemu Peter walikuja kunitembelea
Monaco. Kaka zangu hawa wawili hawakuniambia kama walikua wanakuja.
Lakini damu nzito kuliko maji nikawapokea. Walifika asubui sana mimi
nikiwa naelekea kwenye mazoezi.Nilivyorudi tulikua na mazungumzo na
walisema wanataka kuanzisha biashara ya magari. Ki ukweli biashara hiyo
inahusisha pesa nyingi sana lakini niliwambia nitawasaidia nikipata
malipo yanayofuata.
Wakati huo Thierry Mangwa alikua anaishi kwenye nyumba yangu
kwasababu alikua ana matatizo binafsi so ikabidi tukae wote.Siku moja
narudi kutoka mazoezini nikamkuta analina na hajawai kuniambia kwamba
hata kaka zangu hawakuniambia.Siku nyingine rafiki yangu Padjoe alikuja
kunitembelea na wakati anaondoka nikampa €500. Kaka yangu Kola alivyojua
hivto alikasirika sana. Alikua hajaelewa kwanini nimpe rafiki pesa na
sio yeye. Sababu ilikua ni simple, pesa aliyokua anataka Kola ilikua ni
nyingi.
Siku moja nilikua nimechoka sana baada ya mazoezi nikaamua kulala,
nilivyoamka nikakuta kisu shingoni mwangu na kaka zangu walikua wanapiga
kelele kwamba nawapotezea muda.Nikawauliza hii ndio njia ya ku-solve
tatizo, basi niueni na mchukue pesa. Basi wakaniacha na kuweka kisu
chini.
Mama akanishauri niite polisi na nikafanya hivyo lakini damu nzito kuliko maji nikaacha yapite.
Baada ya mwezi nikarudi Togo nikashangaa mama yangu akibwatukia
kwanini nimewaita polisi kisa kaka zangu wakati yeye ndie aliyenishauri
hivyo. Akasema mimi ni mtu mbaya kwenye familia.
Kila muda nikirudi Togo watu wananiuliza kwanini kaka yangu Kola harudi
kutembelea nyumbani baada ya miaka yote aliyoenda Ujerumani.Nikamnunulia
ticket ya ndege na kumsafirisha hadi nyumbani kwa gharama zangu
mwenyewe.
April 22, 2005 baba yetu alifariki na kabla ya hapo aliniambia
nihakikishe msiba wake usiwe sehemu ya masikitiko bali tufurahie na
kujivunia maisha yake hapa duniani. Mimi nikanunua ticket kwa ajili ya
kaka zangu wote na tukaenda Togo na nikafanya kama baba alivyoseama.Kola
anaejiita baba wa familia alifanya nini kwenye huo msiba licha ya kukaa
ujerumani miaka yote.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment