News
Loading...

LIST YA WANAMICHEZO MATAJIRI IMETOKA, JE MESSI NA RONALDO NANI ZAIDI?

  Jarida namba moja kwa masuala ya fedha – Forbes kutoka nchini Marekani limetoa listi ya wanamichezo walioingiza fedha nyingi zaidi duniani katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Hii ndiyo orodha kamili ya top 5 ya wanamichezo walioingiza fedha nyingi kwa kipindi hicho:
 1. Floyd Mayweather Jr.

Mapato yote: $300 million
 Malipo ya Ndondi: $285 million 
Matangazo: $15 million 

Mapato haya ya $300 million kwa mwaka yanavunja rekodi mapato makubwa zaidi aliyowahi kuingiza mwanamichezo yoyote kwa kipindi cha mwaka 1. Rekodi iliyopita ilikuwa ikishikiliwa na Tiger Woods aliyeingiza $115 million mwaka 2008.
2. Manny Pacquiao
 
Mapato ya Jumla: $160 million
Mshahara: $148 million
Matangazo ya Biashara: $12 million

Fedha aliyolipwa Pacquiao $125 million kwenye pambano dhidi ya Mayweather ilikuwa mara nne zaidi ya fedha aliyopata katika pambano lake lilopita dhidi ya Chris Algieri. Mapato mengine yametokana na Nike, Foot Locker, Wonderful Pistachios, na matangazo mengine ya biashara.
3. Cristiano Ronaldo
          
Mapato ya Jumla: $79.6 million
Mshahara/Posho/Bonasi: $52.6 million
Matangazo ya Biashara: $27 million

Akiwa bado anashikiliwa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia Ronaldo ndio mwanasoka anayelipwa fedha nyingi duniani mbele ya mpinzani wake Lionel Messi. 
 4. Lionel Messi

Mapato ya Jumla: $73.8 million
Mshahara/Posho/Bonasi: $51.8 million
Matangazo: $22 million

Mwishoni mwa mwaka jana Barcelona walimpa Mess mkataba wenye thamani ya $9 million kwa mwaka – ambao unamfanya anaondoka na $50m kwa mwaka.
  5. Roger Federer
 
Mapato ya Jumla: $67 million
Mshahara: $9 million
Matangazo: $58 million 

Pamoja na kutokuwa na mafanikio makubwa uwanjani, lakini Federer, bingwa wa mara 17 wa mataji makubwa ya tennis anaingiza fedha nyingi kutokana na mikataba yake ya kibiashara kama Nike, Rolex na Credit Suisse. Na Mwaka uliopita aliongeza mkataba wake na Mercedes Benz kwa miaka 3.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment