News
Loading...

DIAMOND PLATNUMZ AINGILIA KATI UGOMVI WA LOWASSA NA MAGHUFULI

August 25 mwaka 2015 ni siku ambayoatanzania wote tutapiga kura kumchagua Rais ambaye ataiongoza Tanzania kwa miaka mitano ijayo lakini pia tutapiga kura kuchagua Madiwani pamoja na Wabunge watakao wakilisha wananchi kwenye shughuli mbalimbali za kiserikali na kuleta maendeleo kwenye nchi.
Lakini pia homa ya uchaguzi imekuwa kubwa hasa kwa vyama viwili ambavyo vinaonekana kutoana jasho ni CCM na UKAWA kupitia mgombea wake kwa tiketi ya Chadema, CCM mgombea wao ni John Maghufuli huku Ukawa wakiwakilishwa na Edward Lowassa ambaye alikatwa kwenye kura za maoni ya kugombea tiketi ya Urais kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM).
Tayari mpaka sasa tumeona baadhi ya mastaa wa Tanzania wakiweka wazi watu wanaowakubali kati ya hawa wawili, miongoni mwao ni Wema Sepetu aliyeweka wazi kumsupport Magufuli, mwigizaji Jackline Wolper na Aunty Ezekiel wanamsupport Edward Lowassa na sasa ni Diamond kaweka wazi.
Diamond anamsupport John Pombe Magufuli na kayaandika haya >>> Iwe Msanii, Mtangazaji, ama Mwanamichezo, ila Kila Mtanzania anahaki ya Kuchagua kiongozi anaeamini ni Bora, Mchapa kazi, Mwenye Afya na Msimamo ili kutuendelezea Nchi yetu… Kwa Uchunguzi na tathmini niliyoifanya tangu hizi mambo za Kampeni zianze nimegundua na kuamini kuwa huyu ndio Jembe’
Kwenye sentensi ya pili Diamond akaandika >>> ‘Nitakuandikia na kukupostia ushahidi kukuthibitishia kwanini nimeona John Magufuli Pombe ndie anaefaa… unapohisi na wewe una fact za kumtetea umtakaye karibu uniambie hapo halaf na mi nikumwagie zangu, ila usijisumbue Matusi coz hayatokusaidia wala kunisaidia kunibadilisha akili yangu kwa sababu sanasana ntakuona Huna akili Maana nishayazoea, nipe fact zako nami nikupe zangu ili pamoja Tujenge nchi….. #HapaKaziTu #Ccm

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment