News
Loading...

DZEKO ATUA RASMI LIGI YA SERIA A YA ITALIA

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Edin Dzeko amejiunga na klabu ya ligi ya Seria A nchini Italia AS Roma kwa mkopo, klabu hiyo imetoa kitita cha pauni milioni 2.9 na fedha nyengine pauni 7.9 zikitarajiwa kulipwa iwapo uhamisho huo utabadilika na kuwa wa kudumu.
''Nimekuja hapa kushinda mataji, ninaweza kuahidi kitu kimoja kwamba nitajitahidi vilivyo katika kilabu hii''. alisema Dzeko
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na kilabu ya Manchester City akitokea Wolfsburg ya Ujerumani mnamo mwaka 2011 kwa pauni milioni 27.
Meneja wa Man City Manuel Pelegrini hivi karibuni alikiri kwamba Dzeko alikuwa na uwezo mkubwa kuondoka katika Etihad kufuatia usajili wa Raheem Sterling kutoka Liverpool kwa kitita cha pauni milioni 49.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment