News
Loading...

MCHIZI MOX ATOROKA NA MKWANJA WA DESIGNER!!!


Msanii wa hip hop anayewakilisha kundi la 'Wateule' Taikuni Ally maarufu kama Mchizi Mox ameingia kwenye tuhuma ya kuingia mitini na pesa ya designer anayejulikana kwa jina la Katona. Taarifa zinasema kuwa Mchizi Mox alipewa pesa kwa ajili ya kuperform kwenye Fashion Show  ya ‘ZIP SUTI’ lakini msanii huyo hakutokea.
Kiukweli alichonifanyia Mchizimox sijakipenda kwasababu tumekubaliana kabisa kuwa aje kwenye Fashion Show yangu ya ‘Zip suti Fashion tarehe 8 August, 2015 pale Regency Hotel Mikocheni Jijini Dar kufanya show lakini Mchizi Mox hajatokea wakati nilikuwa nimempa hela yake yote, ambayo ni Elfu 50. Nampigia simu hapokei, nimemtumia SMS anirudishie basi hela yangu hajibu, yaani nashindwa hata kumuelewa mpango wangu ni kuifikisha kwa Soud Brown coz alicho kifanya sio powa hata kidogo, bora hiyo pesa ingesaidia mambo mengine, udhibitisho ninao hela nimemtumia kwenye Tigo pesaAlisema Katona
Lakini pia tulimtafuta Mchizi Mox kwa njia ya simu na haya ndio aliyosema kuhusiana na tuhuma hiyo inayomkabili kutoka kwa designer Katona.
Mchizi Mox: Hello
Mwandishi: Yea inakuaje Mchizi Mox
Mchizi Mox: Poa nambie
Mwandishi: Fresh, nasikia umekimbia na pesa za designer, ambazo ulitakiwa kwenda kuperform kwenye Fashion Show ya ‘Zip Suti’ jana vipi tatizo nini?
Mchizi Mox: “Daah! yaani nilipatwa na majanga kaka siwezi kukimbia wala kupoteza uaminifu wangu, ilikuwa hivi wakati natoka zangu home naelekea kwenye hiyo show nilipata ajali ya gari maeneo ya Kinondoni tukapelekana polisi kwa ajili ya hiyo ajali iliyotokea, hatimaye ikaonekana kuwa mimi ndio ninamakosa nikawa nimewekwa ndani usiku huo huo hadi time hii ndio nimetolewa ‘Oystabey Polisi’ hata home bado sijafika.
Nataka nikifika nioge then nimcheki Designer Katona” Mchizi Mox pia aliongeza kuwa  “kwanza nilikuwa namsaidia maana ni Show ambayo hatukuandikiana hata mkataba tulifanyiana kishikaji tu lakini sikukusudia kwa lililotokea.” Alisema Mchizi Mox


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment