Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mrisho Khalfan
Ngassa amesaini mkataba wa miaka minne kuichezea timu ya Freestate Stars
inayoshiriki ligi kuu ya
soka nchini Afrika Kusini maarufu kama PSL .
Ngassa amesaini mkataba huo siku chache baada ya kuisaidia klabu yake
aliyoitumikia kwa muda mrefu ya Dar es salaam Young Africans kutwaa
ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara .
Ngassa amekuwa akisakwa na timu hii ya Afrika Kusini kwa muda mrefu
ambapo iliwahi kutuma ofa ya kumsajili tangu msimu uliopita lakini Yanga
waliikataa ofa hiyo kwa sababu ilikuwa ndogo .
Mrisho Ngassa amekuwa akisakwa na timu nyingi za nje ambazo
zimevutiwa na uwezo wake na kwa nyakati tofauti ofa kadhaa zimewahi
kutumwa kwenye klabu ya Yanga kwa ajili yake .
Klabu za Al Mareikh ya Sudan pamoja na Seattle Sounders ya Marekani
zimewahi kumtaka Ngassa na Sounders wamewahi kumpa nafasi ya kufanya
majaribio katika mchezo dhidi ya Manchester United miaka kadhaa
iliyopita .
Ngassa huenda akaungana na mchezaji mwenzie wa Yanga na timu ya taifa
Simon Msuva ambaye hivi karibuni alifanya majaribio na klabu ya Bidvest
Wits na kama timu hiyo ikiridhishwa na kiwango chake huenda akasaini
mkataba .
0 comments :
Post a Comment