News
Loading...

HUYU NDIYE MRITHI MPYA WA BLATTER


Wakati uchaguzi wa kumpata Rais mpya wa FIFA ukitarajiwa kufanyika february mwakani, Rais wa shirikisho soka Ulaya (UEFA) Michel Platini anatarajiwa kutangaza rasmi nia yake ya kuwania urais wa FIFA.
Platini ambaye mpaka sasa anaungwa mkono na mashirikisho ya soka kutoka mabara manne atakuwa mgombea wa nafasi hiyo wakati uchaguzi wa shirikisho la soka duniani utakapofanyika februari 26 mwakani.
Rais wa FIFA kwa sasa Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 ameliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 na anatarajia kustaafu mwezi Februari kutokana na kashfa ya ufisadi  ambayo imelikumba shirikisho la FIFA.
Na Platini anapigiwa upatu kumrithi.
Baadhi ya mashirikisho yanayomuunga mkono Platin ni pamoja na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, shirikisho la soka kusini mwa Marekani Conmebol, shirikisho la kaskazini America ya kati na visiwa vya Carebean, Concacaf na  la Asia AFC.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment